Kimenuka! Yondani Ajulikani Alipo Yanga Yaitisha Kikao cha Dharura

Kimenuka! Yondani Ajulikani Alipo  Yanga Yaitisha Kikao cha Dharura
WAKATI Klabu ya Yanga imeitisha kikao cha dharura na wachezaji wote 10 waliomaliza mikataba yao, kinachotarajiwa kufanyika leo Jumatano, Mei 30, 2018 jijini dar es Salaam lakini beki wao Kelvin Yondani hawajampata wala hawajui aliko.

Yanga wameitisha kikao hicho ikiwa ni siku moja kabla ya safari kuelekea Kenya kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup, ambapo wataondoka kesho, lekini taarifa zinaeleza kuwa Yondani, ametimkia kusikojulikana.

Yondani hajacheza mchezo wowote tangu agungiwe na Bodi ya Ligi ya TFF baada ya kumtemea mchezaji wa Simba, Asante Kwasi katika mchezo uliowakutanisha watani hao wa jadi, Simba na Yanga, Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amelitolea ufafanuzi kuhusiana na kutopatikana kwa Yondani akieleza kuwa amepatwa na matatizo ya kifamilia hivyo atarejea kikosini siku yoyote.
Mkwasa amesema suala la mchezaji kutokuwa hewani kupitia simu yake haina maana ya kwamba hawezi kuonekana na akieleza kuwa ni jambo la kawaida pekee. Mbali na hilo, Mkwasa amesema Yondani bado ni mchezaji wa wao kwa kuwa bado ana mktaba na Yanga licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa Simba wanamuwinda kwa ajili ya kumsajili.
Yondani alifunguliwa kifungo chake kalba ya mechi dhidi ya Azam kufuatia kitendo chake cha kumtemea mate Kwasi katika mchezo dhidi ya Simba ambao Yanga walikubali kichapo cha bao 1-0, lakini juzi Jumatatu, TFF ilimfungulia kifungo hicho.
Aidha, Mkwasa amesema Majigambo ya Simba kwamba wana fedha ni propaganda tu kwavile wametwaa ubingwa, lakini wachezaji wakiulizwa watasema ukweli, hali ni ngumu kiuchumi kwa klabu zote.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad