Ukiambiwa kiswahili ndio lugha ya kwanza ya asili barani Afrika ambayo inapendwa zaidi Ughaibuni bila shaka utakubaliana na kauli hiyo, Kwani tayari lugha hiyo imeanza kutumika hata katika mazingira ambayo watu wengi wasingeweza kudhania.
Nchini Uhispania ukurasa rasmi wa Instagram wa Ligi Kuu Soka nchini humo La Liga umetumia lugha ya kiswahili kwenye Insta Stories ambapo uliweka picha zaidi ya tatu zote zikiwa zimewekwa picha zilizosindikizwa na maelezo ya kiswahili.
Posti ya kwanza kwenye Insta Stories La Liga waliweka picha ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Atonio Griezman na kuandika “Mambo vipi? La Liga inaongea kiswahili“.
Posti ya pili waliweka picha ya staa wa Barcelona, Lionel Messi na kuandika “Barceolena wametwaa wa 25 katika historia ya La Liga“.
Posti nyingine iliyofuata ilikuwa ni ya mshambuliaji wa Villareal, Carlos Bacca ambapo waliandika “Carlos Bacca (@goleador70) amefunga Hat-Trick yake ya kwanza na Villareal”
Na posti ya mwisho waliweka picha ya mchezaji wa Real Betis na kuandika Caption ndefu iliyosomeka “Real Betis wanaweza kucheza tena kwenye Europa baada ya kutocheza kwa miaka mitano”
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Lugha ya kiswahili kutumika kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kwenye Ligi kubwa barani Ulaya kama La Liga.