DAR: Halmashauri ya Jiji na Menejimenti ya Kampuni ya UDART zinafanya majadiliano ya kukihamisha kituo cha Mabasi ya Mwendokasi(UDART) kutoka Jangwani na kukipeleka katika kituo cha Mabasi ya Mikoani Ubungo(UBT)
Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita, amesema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari ya Mwendokasi yasiendelee kuharibika katika kituo cha sasa cha Jangwani kutokana na kukubwa na mafuriko
Aidha, Halmashauri ya Jiji ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini
Meya Mwita aliongeza kuwa Serikali Kuu imetoa Tsh. Bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha mabasi yaendayo mikoani, kitakachojengwa Mbezi Mwisho