Kituo cha Umoja wa Mataifa Kuhamishiwa Kenya Kutoka Uganda....Yoweri Museven Agoma


UGANDA: Bunge la nchi hiyo limepinga mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuondoa kituo chake cha Kikanda kilichopo Entebbe na kukipeleka mjini Nairobi, Kenya
-
Spika wa bunge Bi. Rebecca Kadaga ameteuwa kamati ya bunge ya maswala ya mambo ya nchi za nje ikiongozwa na mbunge Theodore Sssekikubo kulifuatilia swala hilo
-
Aidha, Rais Yoweri Museveni amemuandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres barua kuelezea kutoridhia na kupinga pendekezo hilo la kuondolewa kwa kituo hicho
-
Nairobi ndiyo mji uliopendekezwa kuwa makao ya kituo kipya cha Umoja wa Mataifa Afrika katika ripoti ya Kamati ya Ushauri wa Utawala na Maswala ya Bajeti(ACABO). Mji wa Budapest nchini Hungary umependekezwa kwa ajili ya kituo cha Ulaya
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad