Korea Kasikazini Yasikitishwa Hatua ya Trump Kujitoa Katika Mazungumzo....... Yasema Ipo Tayari Kukutana Naye Wakati Wowote

Korea Kasikazini Yasikitishwa Hatua ya Trump  Kujitoa Katika Mazungumzo....... Yasema Ipotayari Kukutana Naye Wakati Wowote
Korea Kaskazini imeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya rais Donald Trump kujitoa katika mazungumzo yaliyopangwa kufanyika juni 12 huko Singapore.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari nchini humo, uamuzi huu umekuwa kinyume na matarajio ya dunia.

Inadaiwa kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un alikuwa amefanya jitihada zote katika maandalizi ya mkutano huo na kwamba Pyongyang ilikuwa tayari kuhakikisha tofauti zilizopo kati ya taifa lake na Marekani zinasuluhishwa kwa namna yoyote na popote, lakini Trump mwenyewe amesema uwezekano wa kufanyika mazungumzo hayo bado upo.

Taarifa hizo pia zimeleta mshtuko kwa jumuiya ya kimataifa, ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, ameelezea kuguswa kwake na hatua hiyo ya Marekani huku naye rais wa Korea Kusini Moon Jae-In akitoa wito kuwepo kwa mkutano wa dharura wa viongozi wa juu wa usalama kuhusiana na suala hilo.

Marekani imeghadhabishwa na hatua ya Korea kaskazini kufanya mazoezi juu ya rasi hiyo katika siku za nyuma
Mkutano huu ungejadili namna ya uondoaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea kufuatia mkutano wa Korea zote mbili uliofanyika mwezi April mwaka huu.

Hata hivyo yapo baadhi ya mambo yanayotajwa kama dosari zilizo jionyesha kuelekea mazungumzo hayo na hasa kauli za kushinikiza msimamo wake ndani ya barua aliyomuandikia kiongozi wa Korea Kaskazini baada ya kuwa na mazungumzo na rais wa Korea kusini Moon.

Washington pia inailaumu Pyongyang kwamba haikuwa imara katika maandalizi na kwamba pale maofisa wa Marekani walipopanga kukutana na wanadiplomasia wa Korea kaskazini hawakutokea, dalili zilizokuwa mbaya kuelekea mazungumzo haya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad