Moja ya stori iliyojitokeza katika magazeti ya Tanzania leo May 27, 2018 ni kuhusu taarifa zinazosema Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana amejiuzulu ambapo taarifa hizo hazikuthibitishwa na mtu yoyote mwenye mamlaka ndani ya CCM.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete baada ya kuona taarifa hizo katika magazeti ambazo zimewaacha watu na sitofahamu ameamua kulitolea ufafanuzi suala hilo katika ukurasa wake wa Instagram.
“ Isiwashtue. Ni utaratibu wa kawaida hasa inapofika kipindi kama hiki cha kuchagua Kamati kuu ya Chama Chetu CCM ( Kwa mujibu wa KATIBA) ; Wajumbe wote wa KAMATI KUU ukiondoa wale wanaoingia kwa Nafasi zao UJIUZULU Ujumbe wao ili kumpa nafasi MWENYEKITI Ateue Majina ambayo yatapelekwa HALMASHAURI KUU kupigiwa kura ili kupata KAMATI KUU Mpya”.
“ Kiutaratibu hata Sekretarieti nayo inakuwa ndani yake japo kwa mujibu wa KATIBA, Mwenyekiti anapewa Mamlaka ya kutangaza au kutotangaza kama ataendelea nayo ileile au La.” Ridhwan