DAR: Viwanda vinne vikubwa vya kuzalisha mafuta ya kula vinadaiwa kusitisha uzalishaji kwa takribani mwezi mmoja sasa baada ya kuzuiwa kwa meli mbili zenye mafuta ghafi katika bandari ya dar
Mwenyekiti wa Chama cha Watengeneaji mafuta ya kupikia Tanzania, Hussein Kamote amesema viwanda hivyo vinatengeneza mafuta ya kula ya kutokana na mchikichi na kukidhi mahitaji ya zaidi ya 80% ya watanzania
Amesema mafuta hayo yanayoagizwa kutoka Indonesia na Malaysia yapo bandarini mpaka sasa kwa kuwa TRA imekataa kuyatoa
Aidha amesema kusitishwa kwa uzalishaji kumeathiri zaidi ya wafanya kazi 4000 ambao kwa sasa inabidi wasiende kazini kwa kuwa hakuna uzalishaji