Kwangwaru ya Harmonize Yakimbiza Chati za BBC Radio

Kwangwaru ya Harmonize Yakimbiza Chati za BBC Radio
Harmonize amefanikiwa kuingiza ngoma yake ya Kwa Ngwaru kwenye Top 5 za Afro Boss Airline DNA za kipindi cha Destination Africa kinachoendeshwa na DJ Edu kupitia BBC Radio One Xtra.

Wimbo huo umefanikiwa kushika namba mbili kwenye chati hizo wakati namba moja ikishikiliwa na Davido kupitia wimbo wake mpya wa Assurance.

Wiki iliyopita wimbo huo ulishika namba tano kwenye chati hizo.

Wasanii wengine walioingia kwenye chati hizo ni Shado Chris (Kitadi), Bils na Giggz (Loudah) na Da Capo (Take It All).

Top Post Ad

Below Post Ad