Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma za jamii, Charles Nzase amesema Lulu anaungana na wafungwa wengine 10 wanaofanya usafi wa mazingira wizarani hapo.
Amesema kila siku mwigizaji huyo atatumia saa nne kusafisha mazingira kisha ataendelea na shughuli zake nyingine za ujenzi wa Taifa.
Ameongeza kuwa tayari msanii huyo alianza kutekeleza adhabu hiyo tangu jana na kwamba ataendelea mpaka atakapomaliza kifungo chake Novemba, mwaka huu.
“Atapumzika siku za Jumamosi na Jumapili au siku za sikukuu, hatakuwa peke yake kwa kuwa tayari hapa wapo wafungwa wengine tisa wanaofanya kazi za usafi wa mazingira,” amefafanua Nzase.