Maelfu Waandamana ili Rais Ajiuzulu


Maelfu ya raia wa Malawi mwishoni mwa wiki wameandamana kuipinga serikali katika maandamano ya kwanza tangu mwaka 2011.


Maandamo hayo yaliyoandaliwa na mashirika ya kiraia yamefanyika katika miji sita nchini humo kupinga vitendo vya ufisadi na utawala mbovu chini ya Rais Peter Mutharika, ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu 2014.

Katika maandamano ya July 2011 dhidi ya serikali, polisi walifyatua risasi na kuwaua raia 20, mauaji yaliyoishtua nchi hiyo na kusababisha nchi wafadhili kusitisha misaada yao.

Rais wa zamani wa Malawi, Joyce Banda, alirejea nchini humo, Jumamosi iliyopita baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka minne, licha kitisho cha kukamatwa kwa tuhuma za Rushwa.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad