Marekani: Makubaliano ya Nyuklia na Iran ni ya 'Uongo'

Marekani: makubaliano ya nyuklia na Iran ni ya 'uongo'
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo anasema makubaliano muhimu na Iran ya nyuklia 'yalitokana na uongo', baada ya Israel kudai kwamba ina ushahidi kuhusu mpango wa siri wa nyuklia wa Iran.

Amesema inadhihirisha kuwa makubaliano hayo ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani ya mwaka 2015, yalitokana na uongo na sio nia njema.

Rais Trump ameashiria kwa muda mrefu azma yake ya kujitoa katika makubaliano hayo na anatarajiwa kutoa uamuzi katika wiki zijazo.

Mataifa yenye nguvu yanasema Iran imeshinikiza makubaliano hayo na yanapaswa kuendelezwa.

Kwa pamoja Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimeitaka Iran kuheshimu makubaliano hayo
Iran inashutumiwa nini?

Waziri wa wa Israeli Benjamin Netanyahu siku ya Jumatatu ameishutumu Iran kwa kuendeleza mpango wa kuunda zana za nyuklia - mradi uliopewa jina 'Project Amad', na amesema kuwa nchi hiyo imeendelea kupata elimu kuhusu kuunda silaha za nyuklia baada ya mradi huo kuzimwa mnamo 2003.

Hilo lilifuata ufichuzi mnamo 2002 wa kundi la upinzani linaloishi uhamishoni lililosema kwamba Iran inaunda maenoe ya siri ya urutubisha nyuklia kinyume na makubaliano ya nyuklia ambayo Iran ilitia saini kuyatii.


Daima Iran imekana kuunda zana za nyuklia, na ilikubali miaka mitatu iliyopita kusitisha mpango wake wa kuunda nishati ya nyuklia ili kwa upande wake iondolewe vikwazo.


"Nyaraka zilizopatikana na Israel kutoka ndani ya Iran zinaonyesha pasi na shaka kuwa utawala wa Iran ulikuwa hausemi ukweli. Pompeo alisema katika taarifa yake.

"Tumekagua kwamba nyaraka tulizoziona ni za kweli, "alisema akiongeza: "Iran ilificha mpango kubwa wa nyuklia dhidi ya dunia na shirika la kimataifa la nishati ya atomiki (IAEA) - mpaka leo."


Pompeo pia alionya kwamba Marekani sasa "inakagua ufichuzi huo wa nyaraka za siri wa Iran una maana gani kwa siku zijazo".

Trump, ambaye alizungumza wazi kuhusu upinzani wake wa makubalian hayo na Iran yalifikiwa wakati wa utawala wa Obama, amesema ametizama sehemu ya aliyowasilisha Netanyahu na kueleza kuwa hali hiyo 'haikubaliki'.


Kwa upande wake, Iran imekataa madai ya Israel kuhusu kuwepo kwa nyaraka za siri kutoka Tehran zinazothibitisha kuwa bado wanaendelea na mpango wao wa Nyuklia.

Akizungumza na wafanyakazi mjini Tehran kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alikanusha madai hayo na kusema kuwa nchi yake itajibu kama Marekani itafanya maamuzi yoyote ya kuwaumiza.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad