Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amemuonya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuwa asimchezee Rais Donald Trump ikiwa watakutana mwezi ujao.
Pence pia alisema kuwa Trump ana nia ya kuondoka kwenye mkutano huo ambao unapangwa kufanyiwa nchini Singapore.
Kim Jong-un atishia kufuta mkutano wake na Trump baada ya matamshi ya mshauri wa masuala ya ulinzi nchini Marekani John Bolton aliyesema kuwa Marekani itafuata mfumo wa Libya kuondoa zana za nyuklia.
Kingozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi alikubaliana na mataifa ya Magharibi mwaka 2003 kuharibu mpango wake ili apate kuondolewa vikwazo. Miaka minane baadaye aliuawa na waasi walioungwa mkono na nchi za Magharibi.