Na WAMJW-DSM
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imeridhika na maandalizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko ukiwemo ugonjwa wa Ebola katika mipaka yote na viwanja vya ndege nchini
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere
Dkt.Ndugulile amesema amefika hapo ili kuangalia hali ya maandalizi na ufungaji wa mashine za kisasa za utambuzi wa ugonjwa wa Ebola endapo itatokea mtu mwenye ugonjwa huo
Aidha, alisema wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa nchini na kuweka mfumo wa kubaini watu wanaoingia kwa kubaini hali ya joto linaloongezeka kwa mgeni anayeingia na kufanyiwa uchunguzi zaidi.
“tumeweka mfumo wa kuwafuatilia wale ambao watakua wamebainika na joto zaidi mahali watakapofikia na mawasiliano yao ili kujua hali zao na endapo atapata mabadiliko”
Naibu huyo aliongeza kuwa wamewafanyia mazoezi ya kutosha kwa watoa huduma wa mipakani na viwanja vya ndege na pia kuwapatia elimu jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Dkt.Ndugulile ameendekea kusisitiza na kuwatia hofu wananchi kwamba hadi sasa hakuna mtu alobainika kuwa na ugonjwa wa Ebola na hali ya mipaka ya Tanzania ni salama