Mboni, Masele Wapokewa Bungeni

Mboni, Masele Wapokewa Bungeni
Leo Jumatano Mei 23, 2018 Bunge limewapokea wabunge Mboni Mhita (Handeni Vijijini) na Stephen Masele (Shinyanga Mjini) baada ya kushinda nafasi za uongozi katika mabunge ya Afrika.

Mboni alichaguliwa kuwa Rais katika Bunge la Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na kuwashinda wenzake kutoka nchi mbalimbali.

Kwa upande wake, Masele amechanguliwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema leo baada ya kipindi cha maswali na majibu, wabunge hao watapewa nafasi ya kuzungumza bungeni.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad