Akichangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi bungeni jijini Dodoma jana Mei 17, wizara hiyo ilitengewa fedha za maendeleo Sh bilioni nne lakini hakuna fedha waliyopewa.
“Najiuliza kwanini wameiweka hii wizara peke yake na kuitenganisha na Kilimo au ilikuwa kuwatafutia ‘washkaji’ ulaji, maana yake ni kwamba hamtaki kusikia biashara ya wavuvi nchi hii.
“Ng’ombe 300 wamepigwa mnada ila tembo akila shamba la ekari tano mhusika analipishwa faini ya Sh 100,000 kwa ng’ombe mmoja.
“Wafugaji wetu wanapata shida mtapata hela wapi Ulega (Abdallah, Naibu Waziri wa Kilimo) mwaka uliopita hamkupewa hata 100 afadhali mje hata mimi naweza kuwafadhili,” amesema Marwa.