McCain Ampiga Marufuku Trump Kuhudhuria Mazishi Yake

McCain Ampiga Marufuku Trump Kuhudhuria Mazishi Yake
Leo May 8, 2018 Aliyekuwa mgombea urais nchini Marekani Seneta John McCain amesema hataki kumuona Rais wa nchi hiyo Donald Trump akihudhuria mazishi yake.

Mwanasiasa huyo mkongwe mwenye miaka 81 ambaye anasumbuliwa na kansa ya ubongo amesema haoni sababu ya Trump kuhudhuria mazishi yake au hata kulisogelea kaburi lake pindi atakapokuwa amefariki.

Amesema yeye na wenzake zaidi ya wanasiasa 24 wa chama chake cha Republican, walisema hadharani kuwa hawamuungi mkono Trump na walimtaka kumwachia mgombea mwenza Mike Pence nafasi ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Marekani uliopita.

McCain anasumbuliwa na ugonjwa huo tangu Julai mwaka jana na anadaiwa kuendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad