Mchungaji Lusekelo: Kufa Masikini ni Ufala

Mchungaji Lusekelo: Kufa Masikini ni Ufala
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ bado anaamini kuwa Mtanzania kufa masikini ni ujinga na ufala,  hii ni kutokana na rasilimali zilizopo ndani ya nchi.

Mzee wa Upako amesema Tanzania tuna mbuga za wanyama, madini ya Tanzanite, ardhi yenye rutuba hivyo haiwezekani mtu kufa masikini.

“Kufa masikini sio ujinga tuu ni ufala, sasa ufe masikini si fala tuu, halafu ukute ulipata nafasi na fursa mbalimbali huko,“amesema Mzee wa Upako kwenye kipindi cha  Maisha Mseto cha Times FM na kusisitiza.

“Tuna mbuga za wanyama , tuna Tanzanite, tuna almasi, tuna ardhi bora, Tanzania ni nchi ya pili katika Afrika kuwa na mifugo mingi, halafu bado sisi ni masikini? mimi akili haikubali.“amesema Mzee wa Upako na kutoa mfano.

“Kuna nchi moja Singapore wanaendesha nchi yako kwa bandari tu lakini matajiri wanaikimbilia Japan, kwa hiyo mimi siamini Katika umasikini, sisi sio wazima tumerogwa.” amemaliza Mzee wa Upako.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad