Mdogo wa John Heche Aliyeuwawa kwa Kuchomwa Visu Kuzikwa Leo

Mdogo wa John Heche Aliyeuwawa kwa Kuchomwa Visu Kuzikwa Leo
Mkazi wa Tarime, Chacha Suguta (27), anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu akiwa mikononi mwa polisi, anazikwa leo.

Msemaji wa familia ya Suguta, Wegesa Suguta ameiambia Mwananchi kuwa tayari mwili wa marehemu umewasili kijijini kwao Nyabitocho wilayani Tarime .

Suguta ambaye pia ni mdogo wa mbunge wa Tarime, John Heche, alifariki dunia Aprili 27 baada ya kukamatwa na polisi akiwa baa.

Suguta anazikwa wakati familia yake ikitangaza kuukataa msaada wa chakula uliotolewa na  polisi.

"Familia hatutapokea fidia kutoka kwa mtu wala taasisi yoyote. Lakini tunachoomba hili liwe tukio la mwisho raia kufia mikononi mwa polisi, siyo Tarime pekee, bali nchi nzima," amesema Heche

Tayari askari polisi William Marwa amefikishiwa mahakamani akidaiwa kumuua kwa kumchoma kisu Chacha usiku wa Aprili 27 katika tukio lililotokea eneo la Sirari, mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad