Mwaasheria wa Simba Evodius Mtawala ametoa ufafanuzi kwa wanachama waliojitokeza kwenye mkutano baada ya wanachama kupiga kura ya kupitisha katiba mpya.
Mtawala ameelezea namna ambavyo wanachama wanaweza kunufaika na mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ambapo mwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’ atamiliki hisa 49% na nyingine 51% zikibaki kwa wanachama.
“Tunapokuwa na reja ya wanachama 50,000 tukifanya uhakiki wa wanachama tutakuta tuna wanachama labda 10,000. Ili mwanachama ujue thamani yako kwenye klabu ya Simba sasa hivi katika wanachama 10,000, ukichukua bilioni 4 ambayo ndiyo fedha iliyopo ukaigawanya kwa 10,000 utakuta kila mwanachama anathamani ya shilingi 400,000.
“Tunapofungua wanachama wengine 50,000 ina maana tunahitaji wanachama wengine 40,000 ambao hawapo, ili wapate uanachama haitakuwa kama ilivyokuwa utaratibu wa zamani ulivyokuwa unatumika.
“Uanachama wao hautakuwa wa kulipia kadi shilingi 10,000 na shilingi 12,000 kwa ajili ya ada ya uanachama wa mwaka mzima. Watapata uanachama kwa kulipa sawa na stahiki yetu tutakayokuwa nayo, kwa hiyo mtu akija kuingia atanunua hisa atalipa 400,000.
“Ina maana kwamba unaposema unataka kuuza uanachama wako huyu mtu akishapata masharti ile ada anayolipa inayoendana na thani ya hisa zake kwetu kama ni 400,000 akishalipa hapa ile hela haiingii kwenye kampuni hela hiyo unapewa wews yeye nachukua nafasi yako.
“Sasa hivi unaweza kuuza uanachama wako na ukapata stahiki zako.