Mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa, imemnyima dhamana Mkurugenzi wa Kampuni ya MNM, Engineering Service Ltd, Mhandisi Godwin Mshana, kwa tuhuma za kujenga ukumbi wa Chuo Kikuu Mkwawa, (MUCE) chini ya kiwango.
Mshana alifikishwa leo Mei 10, Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa, Iringa, David Ngunyale.
Wakili wa Serikali, Blandina Mnyamba amemsomea mashtaka Mshana na kusema kuwa alitenda makosa hayo kati ya 2010 na 2012.
Amesomewa mashtaka ya kughushi nyaraka za serikali, kujipatia fedha Sh 3 bilioni kinyume na utaratibu na shtaka la tatu ni kuhujumu uchumi katika matumizi ya Sh 2bilioni.
Dhamana ya Mshana imezuiwa na kesi hiyo itasikilizwa tena Mei 22 mwaka huu.
Mei 2 mwaka huu, akiwa katika ziara Chuo Kikuu cha Muce, Iringa, Rais Magufuli aliagiza uchunguzi ufanyike katika ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa chuo hicho, uliogharimu Sh 8 bilioni.
Pia, Rais Magufuli aliagiza, aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho, Profesa Philemon Mushi naye ahojiwe kuhusiana na ujenzi huo.
Mhandisi Aliyetajwa na Rais Magufuli Asomewa Mashtaka na Kunyimwa Dhamana
May 10, 2018
Tags