Mkuchika amesema hayo jana Mei 5, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua programu za shahada za utunzaji kumbukumbu na nyaraka pamoja na uhazili katika Chuo cha Taifa cha Utumishi wa Umma.
Alisema wastaafu wamekuwa wakitumia muda mwingi kufuatilia mafao yao baada ya kustaafu kutokana na uzembe wa maofisa utumishi katika halmashauri mbalimbali na baadaye kuwataka wastaafu hao kufuatilia taarifa hizo wenyewe.
“Sasa anamwachia yule mtumishi kuhangaika kwa hiyo unakuta mtumishi ametoka Mtwara, Mwanza anakuja kufuatilia mafao yake wakati ni kazi ambayo anatakiwa aifanye Ofisa Utumishi.
“Utakuta mtumishi mwingine baada ya miaka miwili au mitatu anakufa bado hajalipwa mafao yake kwa sababu karatasi fulani imekosekana,” alisema Waziri Mkuchika.