Mlela ameyasema hayo kwenye eNewz ya East Africa Television, na kueleza kwamba wao kama wasanii wanatakiwa wajifunze, kwani kitendo cha msanii mkubwa kama yule kukosa matibabu kwa kutokuwa na pesa sio kitu sahihi na inaonesha ni jinsi gani wasanii wako chini kiuchumi, licha ya kazi nyingi na matangazo mbali mbali ambayo amewahi kuyafanya.
“Kiukweli si sahihi inanionesha ni jinsi gani bado tuko chini, kuomba msaada vile ni udhalilishaji, sisi ambao tuko kwenye game na umri unaruhusu tuchukulie kama changamoto tujipange kama binadamu, haya yasiendelee kujitokeza”, amesema Yusuph Mlela.
Kutokana na hilo Yusuph Mlela ameitaka serikali kutia mkono wake na kusimamia haki na kazi za wasanii, ili waweze kuingiza kile ambacho wanakitolea jasho kwa usahihi.