Mtanzania Simon Msuva anayecheza soka la kimataifa nchini Morocco katika klabu ya Difaa El Jadidi, leo amekutana na wachezaji wa kikosi cha Yanga mjini Algiers, Algeria.
Msuva amepataa wasaa wa kuwatembelea wachezaji hao kwa madhumuni ya kuwajulia hali wakiwa wanasubiria mechi ya mkondo wa kwanza ya Kombe la Shrikisho Afrika dhidi ya USM Alger itakayopigwa kesho.
Msuva alikuwa Algiers na kikosi cha Difaa El Jadidi kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo timu yake jana ilikuwa na kibarua dhidi ya MC Alger katika mtananage ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Winga huyo aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kutimkia Uarabuni kujiunga na Difaa ambayo anaitumikia kwa sasa.
Kikosi cha Yanga kesho kitakuwa kinashuka dimbani kwa ajili ya kukipiga na USM Alger, mechi ikitarajiwa kuanza majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.