Mtanzania Akwapua Tuzo ya Uongozi bora Marekani

Mtanzania Akwapua Tuzo ya Uongozi bora Marekani
Leo May 1, 2018 kunayo hii ya kuifahamu ni Chuo Kikuu cha Minnesotan nchini Marekani kimetoa tuzo ya uongozi bora kuhusu kuhudumia watu wenye ulemavu kupitia michezo kwa Mtanzania N’nyapule Madai.

Mtanzania huyo ambaye ni Kamishna mstaafu Msaidizi Ustawi wa Jamii, amepewa tuzo hiyo April 26, 2018 ikiwa ni sehemu ya kutambulika kwa mchango wake hasa wa kuwahudumia watu wenye ulemavu.

“Tuzo hii ni heshima kwetu Special Olympics lakini pia kwa Watanzania kwa ujumla, kikubwa ni serikali na wadau kutuunga mkono ili tuwasaidie watu wenye ulemavu,”amesema Madai

Pia mstaafu Madai ameihasa jamii kutowaficha watu wenye ulemavu kwani wana uwezo wa kubadilisha maisha yao kupitia michezo na kukuza uchumi wa nchi.

“Wapo walemavu tuliowasaidia ambapo wengine wamefanikiwa hadi kuoa, sasa ukimficha mtu kama huyo inakuwa haipendezi,” -Madai
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad