Muigizaji wa Filamu Bongo Rammy Galis Kumpa Mtoto wa Masogange Fungu la Pesa


Muigizaji wa filamu bongo Rammy Galis ambaye aliwahi kuwa kwenye mahusiano na video vixen Agness Gerald aliyefariki hivi karibuni, amekusudia kumpa fungu la pesa Sania mabye ni mtoto wa Agness aliyemuacha, mara baada ya kuzindua filamu yake aliyoigiza naye.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Rammy amesema kiasi hiko cha pesa atahakikisha anakamkabidhi mwenyewe mtoto Sania, ambayo ni stahiki yake kutokana na kazi aliyoifanya marehemu mama yake kwenye filamu ya 'Hukumu' waliyoigiza. “Kwanza nisingependa kutangaza rasmi kiasi ambacho kitamfikia kwa sababu sijui filamu mauzi yake yatakuwaje, lakini mimi kama Ramy Galis nitatoa kile ambacho Mungu atanibariki kupitia filamu hii, kutakuwa na asilimia kadhaa ambazo nitaziweka kwa niaba ya mtoto, na nitakaa chini na famlia ya mtoto wa pande zote mbili watakapokubaliana na sio nibaki nazo mimi, ni haki ya yule mtoto”, amesema Rammy Galis.

Sambamba na hilo Rammy Galis amesema filamu hiyo anakusudia kufanya uzinduzi wake mkoani Mbeya ambako Agness ametokea, na anasubiri msiba upite kabisa ili watu wasije wakasema amefuata kiki ya msiba kufanya kazi zake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad