Mwanaume Ajinyonga kwa Chandalua Baada ya Mkewe Kufariki

Mwanaume Ajinyonga kwa Chandalua Baada ya Mkewe Kufariki
Charles Monene Nyatete miaka 42 amekutwa amejinyonga kwa kutumia chandarua kwenye mti wa mparachichi baada ya mke wake kufariki.

Kwa mujibu wa Chifu wa kijiji cha Nyankami jimbo la Nyamira, Cosmas Mocha amesema kuwa marehemu alitoweka baada ya kupata taarifa za mke wake , Carren Kwamboka Monene  kuaga dunia May 27 akiwa hospitalini.

Mke wa marehemu inadaiwa kuwa alikuwa amelazwa hospitalini kwa kipindi cha wiki mbili kabla hajafariki.

Aidha taarifa ya familia ya marehemu inasema kuwa walianza kumtafuta marehemu huyo baada ya kutoweka May 27 kabla ya kumkuta May 28 akiwa ananing’inia kwenye mti wa mparachichi akiwa tayari amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia chandarua.

Baadaye mwili huyo wa marehemu waliuchukua na kuupeleka mochwari kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kipolisi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad