Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, amesema hayo ofisini kwake leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuelezea kuwepo kwa tukio hilo .
Akisimulia tukio hilo Lucas Myovela, amesema alipigiwa simu na Amina Msuya au Ravness anayefanya kazi ofisi RC Arusha upande wa kutunza kumbukumbu, akimuomba wakutane ili amuelezee tatizo kati yake na rafiki yake wa kiume aitwae Swalehe Mwindadi, ambae nae ni mtumishi ofisi ya mkuu wa mkoa, masijala ingawa kwa sasa anasaidia ofisi ya Itifaki.
Anasema Amina au Ravness, alimsimulia mkasa na kumwambia kuwa hawana maelewano na mwenzake hivyo anaomba suala hilo liandikwe kwenye vyombo vya habari kwa kuwa limeshafikishwa kwa Katibu tawala wa mkoa kwa utatuzi lakini hadi leo hajafanikiwa.
Siku ya Jumamosi, May 12 Amina alimpigia simu Lucas na kumtaka wakutane ndipo Lucas aliposema alikuwa hospital ya rufaa ya KCMC akishughulikia suala la baba yake mzazi kuhamishwa hospital kutoka hospital ya Seriani ya jijini Arusha kwa ajili ya matibabu na hivyo alimwambia hataweza kufika.
Amesema kuwa ilipofika saa 3 usiku Amina aliendelea kumpigia simu ya kumsihi waonane ndipo alipomkubalia na kumweleza kuwa yupo wilayani Arumeru na aliambiwa achukue usafiri wa pikipiki hadi Ngurero, jijini Arusha na alipofika eneo aliloagiziwa alimkuta mwenyeji wake akimsubiri akiwa amesimama nje ya gari na mwenyeji wake alimwambia asubiri kidogo amalize kuzungumza na simu.
Amesema muda mfupi alimuona Swalehe na vijana wengine wawili ambao mmoja wapo alivalia Maski usoni na walipofika Swalehe alimshika mikono na kumfunga kwa kamba na kisha wakasaidiana kumuingiza ndani ya gari.
Amesema wakati amefungwa akiwa ndani ya gari alianza kushambuliwa kwa kipigo kutoka kwa Swalehe ambae alisaidiana na vijana wawili huku Amina akiendesha gari na kuelekea Sakina darajani na kisha kumshusha upande wa pili wa Daraja huku wakiendelea kumshambulia na damu ilipoaanza kutoka walimvua nguo na kumwagia maji ya baridi yaliyokuwepo darajani hapo huku wakimpiga picha za utupu na kumlazimisha awape shilingi 500 000/.
Amesema walichukua kadi ya ATM na walitumia Sime na Bastola ndogo kumlazimisha kuwapatia namba za siri na hivyo mmoja alienda kuchua fedha zilizokuwemo kwenye Account yake.
Amesema wakati hayo yakiendelea Swalehe alikuwa akiwasiliana na polisi aliyepo kituo kidogo cha polisi cha Ngarenaro na walipofika walikuta kituo kimefungwa hivyo alipelekwa kituo kikuu cha polisi jijini Arusha, ambapo walitoa maelezo kuwa wamemkamata mwizi akijaribu kufungua milango ya gari lao kwa lengo la kuwaibia madai ambayo aliyapinga na kueleza tukio zima.
Lucas, anasema wakati alisimulia tukio hilo polisi Swalehe alitoka nje na kuingia ndani ya gari huku akianza mchakato wa picha za utupu za tukio hilo walizozipiga wakiwa Darajani Sakina ndipo polisi walipomfuata na kuchukua simu hiyo kabla hajafanikiwa kufuta picha hizo