Mwigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels amemshtaki Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu ujumbe wa Twitter anaodai ni wa kumharibia jina, wakili wake amesema.
Bi Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, anasema alitishiwa na mwanamume mmoja katika maegesho ya magari mjini Las Vegas na kutakiwa kuacha kuendelea na madai yake kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bw Trump.
Rais huyo wa Marekani alipakia kwenye Twitter mchoro wa mwanamume mshukiwa na kisha kuandika "hii ni kazi ya utapeli kabisa".
Wakili wa Bi Daniel aliandika kwenye Twitter kwamba Bw Trump "anafahamu vyema kabisa yaliyotokea".
"Bw Trump alitumia fursa ya mamilioni ya watu katika taifa hili na kimataifa (wanaomfuatilia katika mtandao huo wa kijamii) kutoa taarifa ya uongo yenye lengo la kumshushia hadhi na kumshambulia Bi Clifford," kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya dola mjini New York inasema.
Kesi hiyo inasema ujumbe huo wa rais ulikuwa wa kumharibia mtu jina kwani ulimtuhumu Bi Daniels kwa "kutekeleza kosa kubwa" - hususan, la kumtuhumu mtu mwingine kwamba alimtishia.
Bw Trump alikuwa amepakia mtandaoni mapema mwezi huu picha ya mchoro wa mshukiwa huyo na kumweleza kuwa "mwanamume asiyekuwepo".
Mwanamke huyo aliambia kipindi cha CBS News kwamba baada ya kutamatika kwa uhusiano wao, mwanamume mmoja alifika alipokuwa yeye na binti yake katika maegesho hayo ya magari Las Vegas na kumwambia "sahau taarifa hiyo, mwache Donald Trump".
Trump amekana kuwa na ufahamu wowote kumhusu Cohen ambaye hapa anaonekana akiingia mahakamani
Kesi hiyo hata hivyo ilisitishwa kwa siku 90, huku jaji akisema kwamba haki za Bw Cohen zingekuwa hatarini iwapo kesi hiyo ingeendelea akiwa bado anachunguzwa.
Mashtaka Maalum Robert Mueller kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 na kwamba taifa hilo lilishirikiana na maafisa wa kampeni wa Rais Trump.