Mwili wa Mbunge Bilago Watolewa Muhimbili Kupelekwa Bungeni Kwaajili ya Kupewa Heshima ya Mwisho

Mwili wa Mbunge Bulago Watolewa Muhimbili  Kupelekwa Bungeni Kwaajili ya Kupewa Heshima ya Mwisho
MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu Kigona (CHADEMA), Kasuku Bilago umetolea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kupelekwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Dodoma kuagwa na wabunge wote.



CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO -CHADEMA

TAARIFA KUHUSU RATIBA YA KUAGA NA MAZIKO YA MHE.KASUKU BILAGO MBUNGE WA JIMBO LA BUYUNGU, MKOA WA KIGOMA

Tunautangazia umma kuhusu ratiba ya kuaga na mazishi ya Mbunge wa Buyungu Mhe.Kasuku Bilago ambaye pia alikuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Magharibi yenye Mikoa ya Kigoma,Katavi na Tabora.

Kwa upande wa Bunge Marehemu alikuwa Naibu Waziri Kivuli katika wizara ya Elimu na Mafunzo.

Baada ya kikao baina ya familia na Viongozi wakuu wa Chama kilichofanyika leo tarehe 27 Mei,2018 ratiba iliyokubaliwa ni kama ifuatavyo;



Jumatatu tarehe 28 Mei 2018 ni ibada fupi na kuuaga mwili katika viwanja vya Karemjee Dar kuanzia saa sita kamili mchana na mwili kupelekwa Uwanja wa ndege, Dar es Salaam.

Tarehe 29 Mei siku ya Jumanne asubuhi mwili utapokelewa uwanja wa ndege, Dodoma na kupelekwa Bungeni ambapo Wabunge watauaga mwili katika viwanja vya Bunge Dodoma. Baada ya hapo mwili utasafirishwa kwa ndege kuelekea Kibondo.



Tarehe 30 Mei siku ya jumatano wananchi wa Jimbo la Buyungu watapata fursa ya kuuaga mwili katika eneo litakalotangazwa baadae.

Alhamisi tarehe 31 Mei, ndio siku ya Mazishi rasmi ambayo yatafanyika Nyumbani kwa Marehemu huko Wilayani Kakonko, Kigoma.



Kwa ratiba hii tunawatangazia rasmi wananchi wote wa Mkoa wa Dar Es Salaam kuwa kesho wajitokeze kwa wingi ili kuweza kumpa heshima za Mwisho katika ukumbi wa Karemjee .
Aidha tunatoa wito kwa Wanachama, wapenzi na Watanzania wote tuendelee kuikumbuka familia ya Marehemu katika Sala na Dua katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mpendwa wao ili Mungu aendelee kuwapa faraja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad