Mzee Akilimali: Waondoke Wachezaji Wote Yanga Lakini si Yondani Sababu Ntalia Sana

Mzee Akilimali: Waondoke Wachezaji Wote Yanga Lakini si Yondani Sababu Ntalia Sana
WAKATI ikitajwa kuwa huenda beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani akatimka ndani ya kikosi hicho, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali, amefunguka kuwa ni bora waondoke wachezaji wote lakini si Yondani, sababu atamwaga machozi.



Yondani, mkataba wake unamalizika ndani ya klabu hiyo na amekuwa akihusishwa kuwa huenda akatua katika Klabu ya Azam ambapo inadaiwa kuwa anahitajika kwenda kufanya kazi na kocha mpya ya timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.



Akizungumza na Cham­pioni Jumatano, Mzee huyo alisema kuwa anaumia sana anavyozisikia taarifa hizo na anamuomba beki huyo kubaki hapo.



Akilimali alienda mbali zaidi na kudai beki huyo amekuwa na msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo.

“Kama hizo taarifa ni za kweli Yondani ataondoka basi binafsi nitalia sana, sababu ni moja, kati ya wachezaji ambao walikuwa wanacheza kwa nguvu kubwa, alijituma bila kuan­galia klabu ipo kwenye hali gani basi ni Yondani.



“Waondoke wache­zaji wote lakini siyo yeye, itaniuma sana, siyo siri kwa jinsi ambavyo nam­fahamu mjukuu wangu, nimekuwa nikiongea naye mambo mengi kutokana na kuipenda timu na kujitu­ma,” alisema Akilimali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad