Mzee wa Miaka 104 Aliyeomba Kujiua, Hatimaye Afanikiwa Kujiua

Mzee wa Miaka 104 Aliyeomba Kujiua, Hatimaye Afanikiwa  Kujiua
Mwanasayansi David Goodall amehitimisha safari yake ya hapa duniani baada ya kujichoma sindano mwenyewe ya sumu iliyochukua dakika moja kuchukua uhai wake.

Mwanasayansi huyo mwenye miaka 104 aliyehitimisha maisha yake ya kuishi hapa duniani alizaliwa jijini London Aprili mwaka 1914 ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza vita ya kwanza ya dunia.

Mwanasayansi huyo mkongwe  alisafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswis kwa ajili ya kujitoa uhai kwa hiari, ingawa alisema anachukizwa na kitendo hicho.

Goodall alishika bomba la sindano yenye sumu na kusukuma kwenye mwili wake, na  ilitumia dakika moja sumu ikaenea mwili na kupoteza uhai wake.

Sindano ambayo aliitumia kujichoma ilikuwa na sumu aina ya Sodium pentobarbital ambayo iliingia kwenye mishipa ya mwanasayansi huyo.

Wasamaria wema walimchangia Dola 20,000  za Marekani ambazo ni sawa na Sh45milioni ili kumsaidia kutimiza azma yake hiyo.

Kabla ya kifo chake alisema kwamba kinachomfanya  aharakishe kufa ni kutokana na kupungua kwa  uhuru unaosababishwa na  umri.

Hata hivyo mwili wake utachomwa moto nchini Uswisi na kisha majivu yatapelekwa nchini Australia.


Tags

Top Post Ad

Below Post Ad