Moja ya mambo yaliyosisimua zaidi katika sherehe ya usiku wa ndoa ya Mwanamfalme Prince Harry na mkewe Meghan Markle, ni pale ambapo biharusi alipokabidhiwa pete aliyokuwa akivaa marehemu Princess Diana ambaye ni mama wa mumewe. Ikumbukwe kuwa hata wakati Prince William (kaka yake Harry) anamwoa Cathy Midleton alipewa zawadi ya mkufu ambao pia ulikuwa ukitumiwa na Prince Dianna.
Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu 200 waliokuwa katika ukumbi wa Frogmore na wengine 100,000 waliruhusiwa kufuatilia sherehe hiyo wakiwa nje ya ukumbi huo.