Ngorongoro Heroes yachezea kichapo, Yajiweka Katika Madhingira Magumu ya Kufuzu

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya vijana ya Mali kwenye mchezo uliomalizika jioni kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Ngorongoro imejiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu hatua inayofuata ikiwa na kazi ya kubadili matokeo ugenini ili iweze kushinda na kufuzu kutokana na kuruhusu mabao ya ugenini kwa Mali.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na waamuzi kutoka Comoro, Soulaimane Ansudane aliyepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera Mmadi Faissoil na Abdoulmadjid Azilani, hadi mapumziko tayari Mali walikuwa mbele kwa mabao 2-1.

Ousmane Diakite alianza kuifungia Mali bao la kuongoza kabla ya Samadiare Dianka kufunga bao la pili wote wakitumia makosa ya walinzi na mlinda mlango Abdultwali Msheri.

Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Paul Peter ndiye aliyeifungia Ngorongoro Heroes bao la kufutia machozi dakika ya 44 akiuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Mali, Youssouf Keita kufuatia shuri la mpira wa adhabu.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad