" Nitaendelea Kusema Ilihali Nipo Ndani ya Bunge Hili" Bashe

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussen Bashe (CCM), amesema kwamba Bungeni kumekuwa na siasa mbaya za kuamini kila anayesema ukweli anamchukua Rais Magufulii ilihali anaisaidia serikali kuikumbusha mapungufu yake na kuyafanyia kazi ili kuboresha utendaji na kupeleka maendeleo kwa wananchi.

Bashe amesema hayo Bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa, Mei 18, 2018 wakati akichangia hoja kuhusu Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa bungeni na waziri wake, Luhaga Mpina.

” Sisi hatuna nia mbaya na mawaziri, humu ndani kumekuwa na siasa mbaya sana, kila anayejaribu kusema ukweli anapewa jina kwamba anamchukia Rais Magufuli. Mimi simchukii Rais, nilimchagua kwa kumpigia kura, nilimpigia kampeni kwa siku 60, ninafahamu atakuwa mgombea wangu wa urais mwaka 2020 ndiyo maana nayasema haya.

 “Kama ningejua Rais Magufuli siyo mgombea wangu mwaka 2010 wala nisingejali kusema haya ninayoyasema ndani ya bunge, mimi nitaendelea kusema ilihali nipo ndani ya bunge hili. Naomba hii bajeti irudi, wala siyo kwa nia mbaya….. Bajeti ya Maendeleo iliyotengwa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi mwaka jana ni asilimia sifuri, tunaenda wapi?

“Mvuvi amekataliwa kuvua, option yake ni nini? Tunamtia umaskini mkulima…. Nchi yetu leo mkulima ananyanyasika, mfugaji ananyanyasika, mvuvi ananyanyasika, machinga ananyanyasika, mfanyabiashara ananyanyasika, nataka nikwambie Mhe. Spika, unda kamati, mimi siyo mtaalam wa kanuni,” alisema Bashe.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad