Odinga Awasihi Wafuasi Wake Kumaliza Mgomo

Odinga Awasihi Wafuasi Wake Kumaliza Mgomo
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amewasihi  wafuasi wake wasitishe kampeni ya kususia bidhaa na biashara za kampuni zilizohusishwa kuwa na uhusiano na chama tawala cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta.


Bwana Odinga ametoa tamko hilo leo katika sikuukuu ya Mei mosi zilizofanyika katika mji mkuu wa Kenya jijini Nairobi.

"Tulikuwa na hasira nyingi kwa yale makampuni yaliokuwa yanaunga mkono serikali ya Jubilee. Tulisema ni makampuni ambayo yanatesa watu wetu, ambayo yamekataa kukubali uamuzi wa wananchi na tukasema watu wetu wote wasusie bidhaa za kampuni hizo. Sasa tumeshikana mkono na Uhuru, tumekubaliana kufanya kazi pamoja tusulishe mambo, na tumeweka sasa kamati ya ushauri ya kuleta suluhu ya kudumu" amesema Odinga.

Ameongeza "Kwa hiyo leo hii tunatangaza tunatoa ile amri ya kususia.

Tangazo la kususia bidhaa za wanaotajwa kuwa washirika wa chama tawala lilitolewa Novemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu ambao ulibatilishwa na Mahakama ya juu nchini humo kwa madai kuwa ulikuwa na dosari.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad