Hapo jana Ringtone Apoko aliweka wazi kuwa amenunua gari hilo baada ya kusikia Zari atawasili nchini humo kwa ajili ya event yake, pia kipindi cha nyuma msanii huyo alipopata taarifa za Zari kuachana na Diamond alijitokeza na kueleza ana nia ya kumuoa.
Zari akiwa nchini Kenya amehojiwa na kituo cha Radio, Kiss FM na kueleza kuwa hamfahamu msanii huyo.
“I don’t know ringtone and I have never met him. This is actually news to me. I have over 3.9 million followers on instagram and I wouldn’t know who follows me,” Zari said.
“Simfahamu huyo Ringtone na sijawahi kukutana naye, ndio mara ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Nina watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wananifuatilia, siwezi kujua nani kunifuata na kwa wakati upi,” amesema Zari.
Zari yupo nchini Kenya kwa ajili ya event yake ‘The Colour Purple’ itakayofanyika weekend hii Uhuru Gardens.