Poul Kagame Awawakia Viongozi wa Arsenal .... Amkingia Kifua Wenger

Poul Kagame Awawakia Viongozi wa Arsenal .... Amkingia Kifua Wenger
Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame ameweka wazi kuwa kufanya vibaya kwa Arsenal ni tatizo la uongozi na sio kocha Arsene Wenger hivyo yeye kama shabiki wa timu hiyo ameumizwa na Wenger kuonbdoka bila taji.


Kagame ametumia mtandao wa 'Twitter' kuelezea mapenzi yake kwa klabu hiyo ambayo usiku wa kuamkia leo imeondolewa kwenye michuano ya Kombe la Europa.

''Kuhusu timu yangu ninayoipenda ya Arsenal, ni timu nzuri sana na imekuwa na kocha bora sana ambaye ni Wenger na hakupaswa kuwa na mwisho huu wa kuondoka bila kombe, lawama zote ziwaendee viongozi, lakini nitaendelea kuipenda Arsenal'' amendika Kagame.

Mapema mwezi April, Arsene Wenger alitamngaza kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu baada ya kuifundisha timu hiyo kwa miaka 22 huku akiipatia mafanikio kadhaa.



Kutolewa kwa Arsenal jana na Atletico Madrid kunamaanisha timu hiyo msimu ujao haitashiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao. Arsenal sasa inashika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa EPL na ikimalizia hapo itashiriki Europa msimu ujao.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad