Raia wa Kigeni Wanunua Ndoa Nchini Costa Rica

Raia wa Kigeni Wanunua Ndoa Nchini Costa Rica
Lilikuwa swali rahisi, lakini ni swali ambalo liliweza kumshawishi Maria (Jina la kubuni) kuingia kwenye makubaliano

Mwanamama wa makamo alimpatia mwanamke raia wa Costa Rica (46) kiasi cha dola 175 za Marekani ili aolewe na Mwanaume wa kichina ili aweze kupata makazi kwenye he could get residency in the Central American country.

Wakati huo Maria alikuwa akiishi katika maeneo duni mjini San Jose, nchini Costa Rica, alikuwa anahitaji mno msaada aweze kulisha familia yake.

'' hatukuwa na chochote cha kula'', Maria alisema sababu ya kuridhia.

Katika eneo analoishi usalama ni mdogo.''maeneo haya namna ambavyo hutakuwa na habari nyingi ndivyo utakavyoishi kwa muda mrefu.'' mkazi wa eneo hilo alitahadharisha


Kilichotokea kwa Maria si jambo geni hapa.Mwanasheria au mtu wa kati hufika kuwatafuta watu wenye shida na pesa na kuwashawishi kuolewa na raia wa kigeni ambao hata hawajawahi kukutana.

Maria aliolewa bila hata kuyaacha makazi yake.Aliingia ndani ya gari kisha akaweka saini vyeti vya ndoa na kupata dola 175 kwa makubaliano kuwa akielewa kuwa atapewa talaka mapema iwezekanavyo.

Anasema hayo ni maelezo aliyopewa ''walinionyesha picha ya mwanaume mchina wakaniambia'',Bi Maria unaolewa na mwanaume wa China.'' alieleza.

Kwa Maria,mtu wa kati aliendelea na majadiliano kuhusu bei kisha baadae akarejea na makaratasi kwa ajili ya talaka

Miaka michache baadae, aliolewa na raia wa China kwa sababu ya pesa, kama walivyofanya baadhi ya mabinti wake, na mwenza wake.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad