Rais John Magufuli Atoa Milioni 5 kwa Ajili ya Kuchangia Ujenzi wa Shule Morogoro

Rais John Magufuli Atoa Milioni 5  kwa Ajili ya Kuchangia Ujenzi wa Shule Morogoro
Rais John Magufuli ametoa Sh 5 milioni  kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule katika kijiji cha Mkula mkoani Morogoro.

Rais Magufuli ametoa fedha hizo leo Mei 5 akiwa njiani kuelekea Kilombero kwa ajili ya kuzindua daraja.

Magufuli alisimama katika kijiji hicho baada ya kusimamishwa na wanakijiji wa eneo hilo wakati msafara wake ukielekea katika uzinduzi wa daraja hilo.

Wanakijiji hao wamemueleza Rais Magufuli kuwa wameanza ujenzi wa shule lakini unakwenda kwa kusuasua.

Pia wananchi hao wamelalamika ukosefu wa kituo cha afya katika kijiji hicho.

Rais Magufuli aliwakabidhi fedha hizo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkula(Chadema) na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo.

"Nimewakabidhi wote kwa sababu maendeleo hayana chama, nendeni mkazitumie kwa malengo yaliyopangwa, nataka watoto wetu waende shule,” amesema

"Ole wenu mtumie vibaya, Mimi kutumbua kuko palepale, tunachotaka ni maendeleo naomba tushikamane kwa ajili ya maendeleo.” ameongeza

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad