Rais JPM Atoa Agizo Hili kwa Waziri Majaliwa

Rais JPM Atoa Agizo Hili kwa Waziri Majaliwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwashughulikia viongozi wanaowahamisha watumishi wa Umma bila kuwalipa stahiki zao.


Akiongea leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), mkoani Iringa Rais Magufuli amesema jambo la kuhamisha wafanyakazi bila kuwalipa ameshapiga marufuku hivyo kama kuna kiongozi bado anafanya hivyo ni lazima ashugulikiwe.

''Kama patakuwepo na Mkurugenzi ama kiongozi yoyote anamuhamisha mfanyakazi, awe mwalimu au mtumishi yoyote bila kumlipa posho yake ya uhamisho na wawe bado wanaendelea kufanyakazi, Mh. Waziri Mkuu lisimamie hilo wao wahame moja kwa moja kwenye kazi zao'', amesema.

Awali Risala ya Chama Cha Wafanyakazi nchini TUCTA ilieleza pamoja na kuwepo kwa zuio hilo la Rais, lakini bado wafanyakazi wanahamishwa bila kulipwa stahiki zao jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kazi.

Aidha Rais Magufuli amesisitiza kuwa ikitokea kiongozi anamuhamisha mfanyakazi lazima amlipe stahiki zake kwanza vinginevyo huyo kiongozi ni jeuri na dawa yake ni kumuondoa hivyo Mawaziri wanaohusika walifanyie kazi hilo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad