Rais Magufuli Agoma Kupandisha Mishahara, Sababu Hizi Hapa


Katika Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika Iringa leo Mei Mosi 2018, Rais Magufuli amesema hawezi kupandisha mishahara kwa sasa kama ilivyoombwa na Wafanyakazi kupitia TUCTA kwa sababu fedha zote zinatumika katika kufanya mambo makubwa.

Miongoni mwa mambo hayo ni ulipaji wa madeni mbalimbali, kuajiri watumishi wapya, kutoa elimu bure, kuongezwa kwa bajeti ya afya, mradi wa umeme wa maji wa Stiegler's gorge, Reli ya SGR na ujenzi wa viwanda mbalimbali.

Rais amesema "Kwangu mimi naona hizi hela ni bora kuziweka kwenye miradi kuliko kujiongezea mishahara. Mkitaka hii miradi yote tulioianzisha tuifute ili tujipandishie mishahara mimi sina tatizo hata kujilipa milioni mbilimbili. Kupanga ni kuchagua.

Tukitekeleza hii miradi yote haitachukua muda mrefu mishahara yetu bila kuiongeza na hii si lazima Mei Mosi.

Ningekuwa na hela kwenye chungu zimebaki pale leo ningetamka tu lakini nikitamka nitazitoa wapi? Nina mpango wa kuajiri wafanyakazi 52 elfu, ntawalipa nini? Dhamira yangu inanituma kwamba kusubiri ni kitu kizuri. Hebu tujenge miundo mbinu na kuajiri hawa 52,000"

Rais Magufuli amesema kuwa atawapa nyongeza ya mishahara ya kila mwaka na kwamba nyongeza kubwa itakuwepo kabla ya utawala wake kumalizika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad