RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akiwa ziarani mkoani Morogoro amepata fursa ya kuzungumza na wakazi wa Kijiji cha Mang’ula ambao wamemwelezea kero na changamoto zinazowakwamisha katika maendelo ambapo ameahidi kuzishughulikia huku nyingine akizitatua papo hapo.
Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, Rais aliuliza iwapo kuna shule ya sekondari, wanakiji wakajibu ipo, kuhsu matatizo ya shule hiyo, aliomba mwalimu mmoja ajitokeze kuyasema na kwa vile hakukuwa na mwalimu aliyejitokeza, ndipo akajitokeza mtoto Msangi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo ambaye alimueleza rais kwamba shule yao haina vyoo hivyo akamuomba awasaidie.
Baada ya hapo Rais alitoa pesa taslimu kiasi cha Tsh. Milioni 3 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule hiyo na akiwataka wazazi na wananchi wa kijiji hicho kujitoa na kuchangia ili kusaidia ujenzi huo.
Rais Magufuli yupo ziarani mkoani Morogoro akielekea wilayani Kilombero, ambapo atazindua daraja la Mto Kilombero.