Rais Magufuli Atembelea Chuo cha SUA Morogoro.....Wanafunzi Wafunguka na Kueleza Kero Zao

Rais Magufuli Atembelea Chuo cha SUA Morogoro.....Wanafunzi Wafunguka na Kueleza Kero Zao
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) wametoa ya moyoni mbele ya Rais John Magufuli kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo chuoni hapo ikiwamo uhaba wa mabweni ya wanafunzi na fedha za mikopo.

Wametoa ya moyoni baada ya kiongozi huyo mkuu wa nchi kutoa nafasi kwa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho kueleza mambo mbalimbali wanayokabiliana nayo baada ya kufanya ziara katika chuo hicho kilichopo mjini Morogoro.

Kabla ya Rais kutoa nafasi hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alieleza mafanikio na juhudi zinazoendelea kufanywa na wizara yake ikiwa ni pamoja na kufanikisha utoaji wa mikopo.

Hata hivyo, Emmanuel Gwalaje, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kozi ya wanyama amesema wapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo hawajalipwa fedha katika muhula wa kwanza na wanaishi maisha magumu hadi sasa.

Mhadhiri wa chuo hicho, God Swai amesema wanafunzi wanaporwa mitaani na kukabwa kutokana na uhaba wa majengo ya bweni, huku akiomba kujengwa kwa ofisi za wahadhiri chuoni hapo.

Mbali na maombi ya wanafunzi, pia kulikuwa na maombi ya watumishi, huku Amina Juma akiomba Rais Magufuli kuwafikiria watumishi wa darasa la saba waliofukuzwa kazi.

Amesema yeye ni mtumishi chuoni hapo tangu mwaka 1994, aliyeathirika na kuondolewa kwa watumishi wa darasa la saba, akiomba wafikiliwe upya kutokana na hali ngumu ya maisha mtaani.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad