Rais wa Ufaransa Amtaka Kabila Kuang’atuka Madarakani na Kuandaa Uchaguzi

Rais wa Ufaransa Amtaka Kabila Kuang’atuka Madarakani na Kuandaa Uchaguzi
Rais Emmanuel Macron amemhimiza kiongozi wa DR Congo Joseph Kabila kung’atuka madarakani na kuandaa uchaguzi kama ilivyopangwa Desemba mwaka huu.

Akizungumza alipokutana na Rais wa Angola João Lourenço ambaye yuko ziarani nchini Ufaransa, Macron alitoa wito huo kwa Kabila kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa chini ya upatanishi wa Kanisa Katoliki kwamba uchaguzi ufanyike mwaka huu.

“Tunaunga mkono upatanishi wa kieneo,” amesema Macron katika ikulu ya Élysée Palace akiwa na mgeni wake Lourenço kama alivyonukuliwa na jarida la Kifaransa la Jeune Afrique.

Marais wawili hao walisimamia katika dhamira ya kuunga mkono makubaliano yaliyofikiwa Saint Sylvester kwamba uchaguzi mkuu ufanyike Desemba 23 “ambao Joseph Kabila hatashiriki.” Hata hivyo, Macron aliongeza kwamba Ufaransa “haina haja ya kutoa amri” kwa Kabila nini cha kufanya.


Lakini japokuwa Kabila haruhusiwi kisheria kugombea, hajasema hadharani ikiwa hawezi kujitokeza, hali inayochochea wasiwasi kwamba anaweza kubadili katiba na akagombea tena. Muhula wa utawala wa Kabila ulimalizika Desemba 2016.

Lourenço alimwambia rais mwenzake wa Ufaransa kwamba mazungumzo ya upatanishi yanayofanywa hivi sasa na wakuu wa nchi washirika, “Omar Bongo, Denis Sassou Nguesso, Cyril Ramaphosa, na Paul Kagame” ambao “tunajadili mara kwa mara juu ya mustakabali wa DRC, kama ilivyo kwa hali ya baadaye ya Kabila”.

Amesema: “Makubaliano yaliyofikiwa (katika mkesha wa mwaka mpya) yamepata Baraka za kanisa na chochote kinachokuwa kimebarikiwa lazima kiheshimiwe. Tunamshauri Joseph Kabila kufuata njia hii. Lakini huu ni ushauri siyo sharti.

“Hatuna haki ya kumwambia (Joseph Kabila) kwamba lazima ang’atuke, itakuwa juu ya wapigakura kusema hivyo kupitia sanduku la kura. Lakini tunaamini katika uhalali wetu kuzuia machafuko.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad