HABARI kubwa katika Ulimwengu wa soka leo ni kuhusu ushindi wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania ambayo imeinyuka Liverpool ya uingereza kwa bao 3-1 katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Mabingwa Ulaya na kunyakua kombe hilo kwa mara ya nne mfululizo.
Liverpool katika dakika 15 za mwanzo za mchezo huo walianza kwa kasi kubwa wakilisakama lango la Madrid na kukosa mabao mara kadhaa huku Mo Salah akiwasumbua mabeki wa Madrid hali ambayo wengi waliipa nafasi kubwa ya kuwafunga wapinzani wao.
Mambo yalianza kubadilika kuanzia dakika ya 26 baada ya beki wa Madrid, Sergio Ramos kumchezea rafu mbaya Mo Salah ambayo ilimfanya kushindwa kuendelea na mchezo kutokana na maumivu aliyoyapata begani hivyo kutolewa nje na nafasi yake ilichukuliwa na Adam Lallana.
Mambo yalianza kuwa magumu kwa Liverpool kwaniwalipoteza tension ya mpira kwa muda, hivyo kuruhusu mashambulizi mengi langoni kwao huku wakimiliki mpira kwa asilimia 35 pekee dhidi ya 65 za Mdrid.
Lakini mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika, Madrid walikuwa hawajapata kitu wala liverpool walikuwa hawajafunga.
Dakika ya 51 uzembe wa kipa wa Liverpool Loris Karius uliigharimu timu yake baada ya kuanisha mpira vibaya, ukamgonga Karim Benzema na kuipatia Madrid bao la kwanza.
Bao hilo ni la 56 kwa Benzema na anakuwa mchezaji wa pili wa Ufaransa kufunga katika fainali ya Champions League baada ya Zinedine Zidane.
Dakika ya 55 Sadio Mane aliisawazishia Liverpool na hili likiwa bao lake la 10 katika CL msimu huu na la 20 kwa msimu huu.
Dakika ya 61 Zinedine Zidane alimnyanyua Gareth Bale aliyekuwa benchi na sub ya Gareth Bale ilibadili kila kitu katika mchezo huu.
Gareth Bale alifunga mabao mawili, na mabao ya Bale yanamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kuingia kama sub na kufunga mara mbili na kuufanya mchezo kumalizika kwa Madrid kuibuka kidedea kwa mabao 3-1 huku Zinedine Zidane akiwa kocha wa kwanza kubeba CL mara tatu mfululizo.
Real Madrid wanakuwa timu ya kwanza kubeba kombe la CL mara 3 mfululizo baada ya Bayern Munich 1974-1976, na timu za Uingereza sasa zinakuwa zimepoteza katika fainali 7 za mwisho za Ulaya dhidi ya timu kutoka Hispania.
Pamoja na ubora wao wote, Liverpool wakakubali kipigo cha mabao 3 kwa 0 kutoka kwa Real Madrid.