Baada ya taarifa hizo kuenea, Ridhiwani amesema kuwa yeye hana mpango wa kuchukua nafasi hiyo kutokana na majukumu mengine ya kiserikali yanayomkabili.
Akizungumza na radio EFM asubuhi hii, Ridhiwani ameeleza kuwa yeye si Mwanachama wa Yanga hivyo anakosa kigezo hicho cha kuwania nafasi hiyo ya juu katika uongozi ndani ya klabu hiyo.
Mbali na majukumu ya kiserikali, Ridhiwani ameeleza pia kuwa aliwahi kusemwa na mmoja wa kiongozi wa Yanga miaka kadhaa nyuma akielezwa kuwa hana mamlaka ya kuzungumza chochote kuhusiana na klabu hiyo.
Kitendo cha kuambiwa kuwa hana mamlaka ya kuongea chochote, huku akitajwa kuwa hajalipia kadi ya uanachama ndani ya Yanga, kinamfanya asipate nguvu ya kugombea nafasi hiyo.
Kiongozi huyo amesema ni wanachama na mashabiki ndiyo wamekuwa wakipendekeza agombee na si yeye kuwa amehitaji kufanya hivyo.