Muigizaji na mchekeshaji maarufu bongo Steven Nyerere, amesema anatamani kukutana na Rais Magufuli ili amshauri azime data, ili watu wasitumie mitandao ya kijamii kwa kufanya umbea na kuongea habari za uongo za kuchafuana.
Akizungumza na www.eatv.tv, Steve Nyerere amesema iwapo atapata fursa hiyo atamsahuri Rais Magufuli kufuata wanachokifanya China, ambapo wao wamepiga marufuku utumiaji wa mitandao ya kijamii mbali mbali, na kutumia mitandao mingine ya kwao kwa ajili ya kukuza uchumi wao na sio kwa ajili ya kupiga umbea na kueneza habari za uongo.
“Bado tunahitaji kuwa na mwenendo wa China, nitafurahi sana siku Magufuli akizima data, na nadhani kuna haja ya kumshauri Mheshimiwa Rais, kwa sababu kama tunataka kujenga Tanzania ya viwanda, ni lazima siku moja tuzime data hata mwezi nadhani tutafikia malengo, tena andika kabisa Nyerere anatamani kuonana na Magufuli amnong'oneze kuhusu data, azime tu hata nwezi, ili watu wafanye kazi, amesema Steve Nyerere.
Steve ameendelea kwa kusema kwamba ….. “asilimia 90 wanaishi kwenye mitandao na kubuni vitu ambavyo haviingizi taifa hata pato, nia ni kuliongezea taifa pato, wenzetu China wameendelea kutokana kutoipa nafasi mitandao kuihairbu China yao, wameipa nafasi kwa ajili ya kutangaza biashara na utalii, sasa sisi tumeipa nafasi kwa jili ya umbea”,.
Steve Nyerere ametoa kauli hizo zote kutokana na watu kuzusha taarifa kuwa mke wake amemkimbia, baada ya kugundua amezaa nje ya ndoa na muigizaji Welu Sengo.
Sakata la Kuzaa Nje ya Ndoa Lamvuruga Steve Nterere " Natamani Rais Magufuli Azime Data "
0
May 25, 2018
Tags