''Serikali imeshindwa Kuzuia Bidhaa Feki''-Ngwali
May 13, 2018
Mbunge wa Wawi (CUF), Ahmed Ngwali ameitaka serikali kukiri wazi kwamba imeshindwa kuzuia uingizwaji wa bidhaa bandia nchini licha ya jitihada ambazo serikali inatangaza kuzifanya lakini bado bidhaa hizo zimeeendela kuingia nchini.
Mbunge huyo amesema hayo Bungeni jana Mei 11, 2018 wakati wa kuchangia hoja bajeti ya Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza kuwa polisi ndiyo watuhumiwa wakubwa katika uingizwaji wa bidhaa hizo.
“Serikali iseme tu kama imeshindwa kuzuia bidhaa bandia nchini, lakini polisi ambao unasema katika kitabu chako, mnataka kutumia mpaka Interpol katika kuzuia bidhaa feki, polisi hao wenyewe ndiyo wanashiriki katika mambo hayo ya kuingiza bidhaa feki, sasa hiyo Interpol gani mnataka kutumia? Mheshimiwa Mwijage hilo mlirekebishe” alisema Ngwali.
Mbunge huyo ameongeza kwamba serikali imekua inatumia mifumo mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa mizigo bandarini lakini tatizo la uingizwaji wa bidhaa bandia umeendelea kuwa mkubwa.
Kwa upande mwingine Mbunge Ngwali amesema mahitaji ya gypsum nchini ni makubwa kuliko uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya ndani ambavyo vipo vinne tu na vinauweo wa kuzalisha gypsum milioni tano tu wakati mahitaji ya gypsum nchini ni zaidi ya milioni 10 hadi 12.
Tags