Wakati Tanzania ikipiga hatua ya ununuzi wa ndege tatu aina ya Bombardier Q400 kutoka Canada, tayari nchi ya Ethiopia nayo imeagiza ndege nyingine 10 aina hiyo ili kuimarisha usafiri wa anga nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa kampuni hiyo mnamo Aprili 27, 2018 imeonesha kuwa nchi hiyo nimeshaweka oda ya ndege 10 ambapo oda hiyo inakadiliwa kuwa na gharama ya kiasi cha dola milioni 332 zaidi ya tsh bilioni 736.
Shirika la ndege la Ethiopia ndio shirika la ndege la kwanza barani Afrika kuagiza kwa wingi ndege za Bombardier ambapo hadi sasa inamiliki ndege 22 za Bombardier Q400.
Shirika hilo pia linatumia ndege hizo za Bombadier Q400 kwenye nchi za Togo na Malawi hii ni baada ya kuingia ubia na mashirika ya Asky na Malawi Airline.