Serikali Yaanza Kuwachunguza Waliosafirisha Korosho

Serikali Yaanza Kuwachunguza Waliosafirisha Korosho
Serikali imeanza kufanya uchunguzi ili kubaini watu  walioruhusu kupelekwa Korosho zilizochanganywa na mawe bila ya kuchambuliwa nje ya nchi na uchunguzi ukikamilika serikali itatoa kauli mara moja.


Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Mary Mwanjelwa wakati akijibu swali la Mh. Abdulrahman Ghasia Mbunge wa Mtwara Vijijini aliyetaka kujua ni hatua gani zimechukuliwa kwa wale walioruhusu kusafirishwa kwa Korosho zenye mawe nje ya nchi.

Mh. Mwanjelwa amesema hatua zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na kuwafanyia uchunguzi wa kina wale wote walioripotiwa katika taarifa ya timu ya uchunguzi iliyoundwa na serikali ili hatua stahiki zichukuliwe kwa watakaobainika kuruhusu Korosho zilichongaywa  na kokoto kwenda nje ya nchi .

Hatua zingine zilizochuliwa ni kuitaka Bodi ya Korosho , Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kushirikiana.

Pamoja na hayo Mhe Mwanjelwa amefafanua mikakati iliyoafikiwa na serikali ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa ubora wa Korosho ili kudhibiti uhalifu kama huo .
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad